Friday, July 10, 2015

HIKI NDICHO KILICHOTOKEA LEO ASUBUHI BUNJU KATIKA KITUO CHA USALAMA.



Leo ndio nimeamini kama kwel wananchi wakichoka kwa kutokusikilizwa wanakuwa na maamuzi ya ajabu.
Nilipokuwa nyumbani saa moja asubuhi nilisikia taarifa kwenye redio kuwa kuna mwanafunzi amegongwa maeneo ya bunju shule na wanafunzi wakaamua kufunga barabara ya bagamoyo, mimi nikajua kwa kuwa mda umepita tukio litakuwa limetatuliwa kwa wanafunzi kutolewa barabarni na wahusika kuchukua hatua husika. Cha ajabu mida ya saa 3 natoka nyumbani naenda bagamoyo kwenye shughuli zangu nafika bunju magengeni nakuta foleni na napishana na gari la polisi wakiwa na silaha wakirud na magari hayaendi yamesimama.
Nikashuka nikapanda bodaboda hadi polisi usalama, kufika hapo hizo ni balaa vijana wa kihuni wamechukua tukio kuwa lao kwao  wakawa wanavunja magari na wamevamia kituo cha polisi na polisi hawapo wanafanya wapendavyo.
kweli watanzania tulikofikia ni hatari sana na mbaya zaidi ukikutwa unapiga picha wanakupora simu mbele za watu.
kwa  ufupi hicho kwenye picha ndicho nilichokishuhudia kwa macho yangu.
ijumaa njema.

Angalia hapa video fupi ya tukio.

No comments:

Post a Comment