Thursday, February 25, 2016

ELIMU BURE NI JAMBO LINALOHITAJI KUTOLEWA UFAFANUZI KWA KINA KWA WANANCHI.

ELIMU BURE NI JAMBO LINALOHITAJI KUTOLEWA UFAFANUZI KWA KINA KWA WANANCHI.Nimeshafanya uchunguzi wangu na bado naendelea na uchunguzi kuhusu hii sera ya elimu bure, nimepita baadhi ya shule za serikali zilizopo katika mfumo wa elimu bure kwenye baadhi ya mikoa, kwa kweli kunahitajika elimu ya kutosha hasa kwa wazazi na walezi wa wanafunzi. 
Ukiacha changamoto ambazo walimu wanakutana nazo katika sera hii pia nimekutana na tatizo, kwa mfano hadi mwezi huu wa pili unaisha kuna shule nimepita nimekuta baadhi ya wanafunzi wa hiyo shule hawana madaftari ya kuandikia notisi eti sababu kubwa elimu ni bure, ilibid walimu watumie nguvu za ziada kuwafanya wanafunzi walete daftari. walikuwa wanatumia karatasi kuandikia huku wakisubiri daftari za elimu bure.
Kwa hili moja tu na mengine mengi inahitajika kutolewa maelezo ya kina wazazi na walezi waelewa nini dhana nzima ya elimu bure. vinginevyo hii mimba ikifika mda wa kujifungua atazaliwa mtoto tayari marehemu.
by mimi mtembezi.