Kituo cha runinga cha Al Jazeera kinasema kuwa mmoja wa waandishi wake
wa habari amekamatwa nchini Ujerumani kufuatia ombi la Misri.
Ahmed Mansour, ambaye anafanya kazi na idhaa ya kiarabu ya al Jazeera
alizuliwa alipojaribu kupanda ndege kutoka Berlin kwenda nchini Qatar.
Polisi
nchini Ujerumani wanasema kuwa bwana Mansour amezuiliwa kufuatia
waranti ya kimataifa ya kutaka akamatwe kutoka kwa utawala nchini Misri.
Mahakama nchini Misri ilimhukumu Mansour kifungo cha miaka 15 jela kutokana na mashtaka ya mateso.
Aljazeera imeyataja mashtaka hayo kuwa ya uongo.
No comments:
Post a Comment