Maafisa wa afya nchini Korea kusini wamethibitisha visa vingine vitatu vya ugonjwa wa matatizo ya kupumua au MERS.
Kati ya wale waliopatikana wakiwa na ugonjwa huo ni pamoja na daktari
katika hospitali moja mjini Seoul ambaye ametajwa kuwa kitovu cha
ugonjwa huo.
Wataalam wanasema kuwa visa vyote 170 vilitoka kwenye mahospitali na hakuna maambukizi yoyote katika maeneo wanakoishi watu.
Watu 25 wameaga dunia tangu mlipuko wa ugonjwa huo kuripotiwa barani Asia mwezi uliopita.
No comments:
Post a Comment