Saturday, June 20, 2015

"KUNDI LA AL - SHABAAB LAWAUWA MAAFISA 15 WA USALAMA"


 Wanamgambo wamewaua karibu walinda usalama 15 nchini Somalia baada ya kufanya shambulizi katika mji ulio karibu na mji mkuu Mogadishu.
Maafisa wanasema kuwa wanamgambo wa Al Shabaab kwanza walishambulia kizuizi cha polisi cha Afgoye ambapo waliwaua polisi watatu na kuchukua magari kadha.
Kisha waliwavamia na kuwaua wanajeshi kadhaa.
Al Shabaab wanasema kuwa wameongeza mashambulizi siku za hivi majuzi kwa sababu ni mwezi mtukufu wa Ramadhan.

No comments:

Post a Comment