Saturday, August 22, 2015

ZA MWIZI NI AROBAINI KWEL.

Baada ya kufanya matukio ya kupora kwenye maduka mfululizo maeneo ya Goba, Kuanzia bondeni, wakafanya tena maeneo ya kwa sanga wakaenda tena kwa japhet juu kidogo ya bonden na kuua mzee wa watu asiye na hatia siku yao ikafika jana asubuhi walienda kupora Goba mwisho madole asubuhi na hapo ndipo arobaini yao ilipofikia.
 Samahani kwa picha hizi zinatisha ila ndio hali halisi.





Friday, July 10, 2015

HIKI NDICHO KILICHOTOKEA LEO ASUBUHI BUNJU KATIKA KITUO CHA USALAMA.



Leo ndio nimeamini kama kwel wananchi wakichoka kwa kutokusikilizwa wanakuwa na maamuzi ya ajabu.
Nilipokuwa nyumbani saa moja asubuhi nilisikia taarifa kwenye redio kuwa kuna mwanafunzi amegongwa maeneo ya bunju shule na wanafunzi wakaamua kufunga barabara ya bagamoyo, mimi nikajua kwa kuwa mda umepita tukio litakuwa limetatuliwa kwa wanafunzi kutolewa barabarni na wahusika kuchukua hatua husika. Cha ajabu mida ya saa 3 natoka nyumbani naenda bagamoyo kwenye shughuli zangu nafika bunju magengeni nakuta foleni na napishana na gari la polisi wakiwa na silaha wakirud na magari hayaendi yamesimama.
Nikashuka nikapanda bodaboda hadi polisi usalama, kufika hapo hizo ni balaa vijana wa kihuni wamechukua tukio kuwa lao kwao  wakawa wanavunja magari na wamevamia kituo cha polisi na polisi hawapo wanafanya wapendavyo.
kweli watanzania tulikofikia ni hatari sana na mbaya zaidi ukikutwa unapiga picha wanakupora simu mbele za watu.
kwa  ufupi hicho kwenye picha ndicho nilichokishuhudia kwa macho yangu.
ijumaa njema.

Angalia hapa video fupi ya tukio.

Monday, June 29, 2015

KWA UAMUZI HUU HONGERA NACTE.


NACTE YAVIFUTIA USAJILI VYUO VITATU (3) NAKUVISHUSHA HADHI VYUO KUMI NA SITA (16)
HOTUBA YA KAIMU KATIBU MTENDAJI WA BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE) KUHUSU TAMKO LA BARAZA LA KUVIFUTIA USAJILI BAADHI YA VYUO NA KUVISHUSHA HADHI VINGINE - 24/06/2015
Ndugu waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari, ninayo furaha kubwa kuwakaribisha katika ofisi za Baraza. Lengo la kuwaita hapa leo ni kuwapa taarifa juu ya maamuzi yaliyofikiwa na Baraza ikiwa ni katika jitihada za kuinua ubora wa elimu ya ufundi nchini.
Ndugu Waandishi wa Habari
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Sura ya 129, kwa lengo la kusimamia na kuratibu taaluma zinazotolewa na taasisi na vyuo vva elimu ya ufundi nchini, ambavyo siyo vyuo vikuu au vyuo vikuu vishiriki. Jukumu kubwa la Baraza ni kuendeleza na kuinua ubora wa elimu ya ufundi nchini kwa kusimamia kikamilifu shughuli za kuendesha mafunzo ili tuzo zinazotolewa na taasisi na vyuo ziwe na ubora unaokubalika kitaifa na kimataifa.

Kwa kutumia Sheria na Kanuni za Baraza za Usajili (2001) na zile za Ithibati na Utambuzi (2001), mnamo tarehe 20 Februari 2015, Baraza lilitoa notisi ya siku 30 kwa taasisi na vyuo vilivyokiuka taratibu na vyenye mapungufu makubwa ya Usajili na Ithibati kupitia taarifa yake kwa Umma. Notisi hii ililenga kuzipa taasisi na vyuo nafasi ya kujirekebisha.

Baraza linakiri kuwa taasisi na vyuo vingi kama vilivyoorodheshwa kwenye Jedwali Na. 1, Jedwali Na. 3, na baadhi kwenye Jedwali Na. 5 vimechukua hatua mbalimbali za kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza. Hata hivyo, hadi kufikia leo tarehe 24 Juni 2015 yaani siku 124 baada ya Notisi ya Baraza, kuna vyuo ambavyo havijachukua hatua yoyote ya kurekebisha mapungufu yake kama inavyooneshwa kwenye Jedwali Na. 2 na Jedwali Na. 4.

Tamko la Baraza

Kutokana na mapungufu hayo Baraza limeamua kuchukua hatua kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zake kwa taasisi na vyuo vyote vilivyoorodheshwa katika Jedwali Na. 2 na Jedwali Na. 4 kwa makosa yafuatayo:

a)    Ama kumalizika kwa muda wa  Usajili wa Awali (Preparatory Registration) na Usajili wa Muda (Provisional Registration); au
b)    Kutoanza mchakato wa kupata Ithibati baada ya kupata Usajili Kamili; au
c)    Kumalizika kwa muda wa Ithibati na kutochukua hatua ya kuomba upya Ithibati (re-affirmation); na
d)    Taasisi na Vyuo kuamua vyenyewe kusitisha kutoa mafunzo kwa sababu mbalimbali.

      
Jedwali Na. 1: Taasisi  na Vyuo vinavyoruhusiwa kuendelea na taratibu za Usajili baada ya kutimiza masharti

Na Jina la Chuo/Taasisi
Namba ya Usajili
1
Regional Aviation College – Dar es Salaam REG/EOS/028P
2
Zoom Polytechnic College – Dar es Salaam REG/EOS/030P
3
Gataraye Research and Training Centre – Dar es Salaam REG/EOS/034P
4
Modern Commercial Institute (MCI) – Dar es Salaam REG/BMG/024P
5
Evin School of Management – Dar es Salaam REG/BMG/026P
6
Agape School of Management – Dar es Salaam REG/BMG/027P


Jedwali Na. 2: Taasisi  na Vyuo vilivyofutiwa Usajili na kuzuiliwa kudahili wanafunzi wapya baada ya kutotimiza masharti ya Usajili

Na.
Jina la Chuo/Taasisi
Namba ya Usajili/Maelezo
1
Dar es Salaam College of Clinical Medicine – Kinondoni Usajili wa Awali
2
Ndatele School of Medical Laboratory Sciences – Dar-es-Salaam Usajili wa Awali
3
Institute for Information Technology – Dar es Salaam REG/EOS/014
4
DARMIKI College of Educational Studies Hakijasajiliwa. Kimezuiliwa kudahili wanafunzi

Jedwali Na. 3: Taasisi  na Vyuo vinavyoruhusiwa kuendelea na taratibu za Ithibati baada ya kutimiza masharti

Na.
Jina la Taasisi/Chuo
Namba ya
Usajili
Hadhi Kabla ya
Notisi
Hadhi Baada ya
Notisi
1 Mabughai Community Development Technical Training Institute – Lushoto REG/EOS/040 Usajili Kamili Usajili Kamili
2 Kizimbani Agricultural Training Institute - Zanzibar REG/ANE/027 Usajili Kamili Ithibati ya Awali
3 Civil Aviation Training Centre – Dar es Salaam REG/EOS/006 Ithibati ya Muda Ithibati ya Muda
4 Ardhi Institute – Tabora REG/EOS/010 Ithibati ya Muda Ithibati Kamili
5 Bandari College – Dar es Salaam REG/EOS/018 Ithibati ya Awali Ithibati ya Awali
6 Tanzania Institute of Rail Technology – Tabora REG/EOS/012 Ithibati ya Awali Ithibati ya Awali
7 RETCO Business College (RBC) – Iringa REG/BMG/025 Usajili Kamili Usajili Kamili
8 Aseki Business School – Dodoma REG/BMG/030 Usajili Kamili Usajili Kamili
9 Western Tanganyika College – Kigoma REG/BMG/032 Usajili Kamili Usajili Kamili
10 Law School of Tanzania REG/BMG/040 Usajili Kamili Usajili Kamili
11 Royal College of Tanzania  (RCT) – Dar es Salaam REG/PWF/004 Ithibati ya Awali Ithibati ya Awali
12 Tanzania Regional  Immigration Training Academy  (TRITA) – Moshi REG/PWF/030 Ithibati ya Awali Ithibati ya Awali
13 Morogoro School of Journalism (MSJ) – Morogoro REG/PWF/005 Ithibati ya Muda Ithibati ya Muda
14 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUBa) – Bagamoyo (former Bagamoyo College of Arts – Bagamoyo) REG/PWF/010           Ithibati Kamili Ithibati Kamili
15 Newman Institute of Social Work (NISW) – Kigoma REG/PWF/016 Ithibati Kamili Ithibati Kamili
16 Njuweni Institute of Hotel, Catering & Tourism Management - Kibaha REG/ANE/016 Ithibati ya Awali Ithibati ya Awali
17 Geita School of Nursing – Geita REG/HAS/079 Ithibati ya Awali Ithibati ya Awali
18 St. Gaspar Nursing School – Itigi REG/HAS/090 Usajili Kamili Usajili Kamili
19 Bugando School of Nursing – Mwanza REG/HAS/052 Ithibati ya Awali Ithibati ya Awali
20 COTC Mafinga – Iringa REG/HAS/047 Ithibati ya Awali Ithibati ya Awali
21 Kagemu School of Environmental Health  Sciences – Bukoba REG/HAS/034 Ithibati ya Awali Ithibati ya Awali
22 Mvumi Institute of Health Sciences – Dodoma REG/HAS/011 Ithibati ya Awali Ithibati ya Awali
23 Tanzania Training Centre for International Health – Ifakara REG/HAS/003 Ithibati ya Muda Ithibati ya Muda
24 Mbeya Polytechnic College (former Ilemi Polytechnic College) – Mbeya REG/BMG/031 Usajili Kamili Usajili Kamili
25 Institute of Sports Development Malya - Mwanza REG/PWF/019 Usajili Kamili Usajili Kamili
26 Ruaha Community Development Training Institute (CDTI) - Iringa REG/PWF/028 Usajili Kamili Usajili Kamili
27 Uyole Community Development Training Institute (CDTI) - Mbeya REG/PWF/027 Usajili Kamili Usajili Kamili
28 Institute of Rural Development Planning (IRDP) - Mwanza REG/PWF/043 Usajili Kamili Usajili Kamili
29 Rungemba Community Development Institute (CDTI) - Mufindi REG/PWF/007 Ithibati Kamili Ithibati Kamili
30 Time School of Journalism (TSJ) – Dar es Salaam REG/PWF/013 Ithibati Kamili Ithibati Kamili
31 COTC Machame – Hai REG/HAS/087 Usajili Kamili Usajili Kamili
32 Mwambani School of Nursing – Chunya REG/HAS/089 Usajili Kamili Usajili Kamili
33 Kiomboi School of Nursing – Iramba REG/HAS/091 Usajili Kamili Usajili Kamili
34 College of Health Sciences Zanzibar REG/HAS/095 Usajili Kamili Usajili Kamili
35 Kabanga School of Nursing – Kasulu REG/HAS/023 Usajili Kamili Ithibati ya Awali
36 Kondoa School of Nursing – Dodoma REG/HAS/040 Ithibati ya Awali Ithibati ya Awali
37 Lugarawa School of Nursing  – Ludewa REG/HAS/036 Ithibati ya Awali Ithibati ya Awali
38 Tosamaganga School of Nursing  – Iringa REG/HAS/020 Ithibati ya Awali Ithibati ya Awali
39 Vector Control training Centre – Muheza REG/HAS/031 Ithibati ya Muda Ithibati ya Muda
40 Training Centre for Health Records Technology – Moshi REG/HAS/072 Ithibati ya Muda Ithibati ya Muda
41 Dar es Salaam School of Journalism (DSJ) – Dar es Salaam
REG/PWF/012
Ithibati Kamili Ithibati Kamili
42 Financial Training Centre – Dar es Salaam
REG/BMG/004
Ithibati ya Awali
Ithibati ya Awali


Jedwali Na. 4: Taasisi  na Vyuo vilivyoshushwa hadhi baada ya kutotimiza masharti ya Ithibati

Na.
Jina la Taasisi/Chuo
Namba ya
Usajili
Hadhi Kabla ya
Notisi
Hadhi Baada ya
Notisi
1
Sura Technologies – Dar es Salaam
REG/EOS/019
Usajili Kamili
Usajili wa Muda
2
Institute of Management and Information Technology – Dar es Salaam
REG/EOS/016
Ithibati ya Awali
Usajili wa Muda
3
Techno Brain - Dar es Salaam
REG/EOS/021
Ithibati ya Awali
Usajili wa Muda
4
Ministry of Agriculture Training Institute Igurusi - Mbeya
REG/ANE/009
Ithibati ya Awali
Usajili wa Muda
5
Mbozi School of Nursing – Mbeya REG/HAS/062 Usajili Kamili Usajili wa Muda
6
KCMC AMO Ophthalmology School – Moshi REG/HAS/085 Usajili Kamili Usajili wa Muda
7
KCMC AMO Anaesthesia School – Moshi REG/HAS/094 Usajili Kamili Usajili wa Muda
8
Advanced Pediatrics Nursing KCMC - Moshi
REG/HAS/076
Ithibati ya Awali Usajili wa Muda
9
AMO Training Centre Tanga – Tanga
REG/HAS/049
Ithibati ya Awali Usajili wa Muda
10
CATC – Songea
REG/HAS/054
Ithibati ya Awali Usajili wa Muda
11
CATC – Sumbawanga
REG/HAS/055
Ithibati ya Awali Usajili wa Muda
12
COTC Maswa – Shinyanga
REG/HAS/014
Ithibati ya Awali Usajili wa Muda
13
COTC – Musoma
REG/HAS/033
Ithibati ya Awali Usajili wa Muda
14
Dental Therapists Training Centre – Tanga
REG/HAS/057
Ithibati ya Awali Usajili wa Muda
15
Ngudu School of Environmental Health Sciences – Kwimba
REG/HAS/058
Ithibati ya Awali Usajili wa Muda
16
KCMC AMO General School – Moshi
REG/HAS/096
Ithibati ya Muda Usajili Kamili


Jedwali Na. 5: Taarifa kuhusu Taasisi  na Vyuo vyenye maelezo maalum

Na.
Jina la Taasisi/Chuo
Namba ya
Usajili
Hadhi Kabla ya
Notisi
Hadhi Baada ya
Notisi
Maelezo
1
Lake Teachers College – Singida
REG/TLF/001
Usajili wa Muda
Usajili Kamili Kimeruhusiwa kudahili wanafunzi
2
Patricia Metzger Academy of Health and Beauty – Dar-es-Salaam
REG/PWF/022P
Usajili wa Muda
Usajili wa Muda Kimesitisha kutoa mafunzo
3
Institute of Management and Entrepreneurship Development – Dar es Salaam
REG/BMG/039
Usajili Kamili
Usajili Kamili Kimesitisha kutoa mafunzo
4
Tanga School of Nursing – Tanga
REG/HAS/084
Ithibati Kamili
Ithibati Kamili Haijamaliza muda wa Ithibati
5
ESACS School of Journalism and Business Studies – Dar es Salaam
REG/PWF/044
Usajili Kamili
Usajili Kamili Kimesitisha kutoa mafunzo
6
Fire and Rescue Training Centre – Dar es Salaam. REG/EOS/032P
Usajili wa Muda
Usajili wa Muda Kimesitisha kutoa kozi za muda mrefu. Sasa kinatoa kozi za muda mfupi ambazo hazipitishwi na Baraza (NACTE).

Asanteni kwa kunisikiliza.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
24 JUNI 2015

Sunday, June 21, 2015

"MWANDISHI WA ALJAZEERA AKAMATWA UJERUMANI"

Kituo cha runinga cha Al Jazeera kinasema kuwa mmoja wa waandishi wake wa habari amekamatwa nchini Ujerumani kufuatia ombi la Misri.

Ahmed Mansour, ambaye anafanya kazi na idhaa ya kiarabu ya al Jazeera alizuliwa alipojaribu kupanda ndege kutoka Berlin kwenda nchini Qatar.
Polisi nchini Ujerumani wanasema kuwa bwana Mansour amezuiliwa kufuatia waranti ya kimataifa ya kutaka akamatwe kutoka kwa utawala nchini Misri.
Mahakama nchini Misri ilimhukumu Mansour kifungo cha miaka 15 jela kutokana na mashtaka ya mateso.
Aljazeera imeyataja mashtaka hayo kuwa ya uongo.

"VISA VITATU (3) VYARIPOTIWA HUKO KOREA YA KUSINI"

Maafisa wa afya nchini Korea kusini wamethibitisha visa vingine vitatu vya ugonjwa wa matatizo ya kupumua au MERS.
  Kati ya wale waliopatikana wakiwa na ugonjwa huo ni pamoja na daktari katika hospitali moja mjini Seoul ambaye ametajwa kuwa kitovu cha ugonjwa huo.
Wataalam wanasema kuwa visa vyote 170 vilitoka kwenye mahospitali na hakuna maambukizi yoyote katika maeneo wanakoishi watu.
Watu 25 wameaga dunia tangu mlipuko wa ugonjwa huo kuripotiwa barani Asia mwezi uliopita.

Saturday, June 20, 2015

"KUNDI LA AL - SHABAAB LAWAUWA MAAFISA 15 WA USALAMA"


 Wanamgambo wamewaua karibu walinda usalama 15 nchini Somalia baada ya kufanya shambulizi katika mji ulio karibu na mji mkuu Mogadishu.
Maafisa wanasema kuwa wanamgambo wa Al Shabaab kwanza walishambulia kizuizi cha polisi cha Afgoye ambapo waliwaua polisi watatu na kuchukua magari kadha.
Kisha waliwavamia na kuwaua wanajeshi kadhaa.
Al Shabaab wanasema kuwa wameongeza mashambulizi siku za hivi majuzi kwa sababu ni mwezi mtukufu wa Ramadhan.

WATOTO WAONGO NI WAEREVE!!!!!!!!!!


Wanasayansi nchini Uingereza wanasema kuwa wana ushahidi kwamba watoto wanaodanganya bila mtu kugundua wana kumbukumbu nzuri ikilinganishwa na wale wasiodanganya.
Watafiti katika chuo kikuu cha Sheffield kwa siri walichukua filamu ya watoto wa umri wa miaka sita na saba wakifanya mtihani uliokuwa na majibu ambayo yalikuwa yameandikwa nyuma ya zao.
Wale waliodanganya kuhusu kile waliochofanya walifanya vyema kutokana na uwezo wao kukumbuka walichofunzwa.
Mmoja ya watafiti hao Elena Hoicka alisema kuwa sababu kuu ni kwamba wale wanaodanganya hulazimika kukumbuka ukweli wote pamoja na uwongo.
Je!wewe unamaoni gani?








"MAAFISA WA POLISI WASHAMBULIWA VIKALI HUKO BURUNDI"

Kumekuwa na msururu wa mashambulizi ya maguruneti kuwalenga maafisa wa polisi katika mji mkuu wa Burundi Bujumbura.
Maafisa wa usalama wanasema kuwa takriban polisi 11 walijeruhiwa.
Maguruneti hayo yalirushwa katika maeneo ambayo yaliathiriwa na maandamano ya ghasia kufuatia hatua ya rais Pierre Nkurunziza kutaka kuwania muhula wa tatu.
Maafisa wa polisi wamewalaumu wanaharakati wa upinzani.
Makundi ya haki za kibinaadamu yanasema takriban watu sabini wameuawa na wengine 500 kujeruhiwa tangu maandamano hayo yaanze mnamo mwezi Aprili.

"OBAMA KUZURU NCHINI ETHIOPIA"

Ikulu ya white house nchini marekani imetangaza kuwa rais Barack Obama atakuwa rais wa kwanza wa Marekani aliye madarakani kufanya ziara nchini Ethiopia.

Msemaji wake (Josh Earnest) alisema kuwa ziara hiyo itakuja baada ya ziara ambayo atafanya nchini Kenya ambapo ni nyumbani kwa babake akiwa rais wa marekani.
Ethiopia na Kenya zote zimekuwa kwenye mstari wa mbele katika vita dhidi ya kundi la Al Shabab nchini Somalia.

"MISA YA WALIOUWAWA YAFANYIKA CHARLESTON"

Maelfu ya watu wamehudhuria misa katika mji wa Charleston jimbo la South Carolina nchini Marekani kuwakumbuka waamerika tisa weusi ambao waliuawa kwa kupigwa risasii na jamaa mmoja mzungu walipokuwa kwenye mafunzo kanisani.
 Wakishikana mikono waombolezaji waliimba nyimbo za kujifariji. Viongozi wa wakirsto na wayahudia wametaka kuwepo amani.





Mapema mshukiwa Dylann Roof alifikishwa mahakamani akikabiliwa na mashtaka tisa ya mauaji
Mmoja wa marafiki zake Christon Scriven alisema, Roof alikuwa amesema kuwa angewaua wanafunzi katika chuo kilicho karibu lakini alitulia baada ya kuhojiwa .















WAUWAWA KATIKA DUKA LA POMBE MEXICO

Watu waliokuwa na silaha wamevamia duka moja la pombe nchini Mexico ambapo watu 10 waliuawa.
Wavamizi hao waliwasili kwa magari mawili na kuwafyatulia risasi wateja waliokuwa ndani ya duka hilo katika mji ulio kaskazini wa Garcia.Kisha miili yao ilivuliwa nguo na kuporwa.
Wachunguzi wanadai kuwa wanaume hao walikuwa wamelengwa makusudi na mauaji hayo huenda yanahusiana na tofauti kati ya makundi hasimu.

'KOMESHA MAUAJI YA ALBINO TANZANIA'

Je!!wana Damu tofauti na yako!!!!!,Hapana'wanayo kama yako.na wanamchango mzuuri kwa Taifa letu.KWA PAMOJA 'TOKOMEZA MAUAJI HAYA'

KENYAN SECURITY FORCES BELIEVE ABOUT 100 BRITISH NATIONALS HAVE JOINED AL-SHABAB!!!!!!.

Thomas Evans, 25, from Buckinghamshire, died in the thwarted attack on a military base on 14 June.
Police now say he was also the group's cameraman, and captured images of the incident up until his death.
Kenyan security forces killed 11 gunmen and two soldiers died after the raid in Lamu County, near the Somali border.
Al-Shabab, an al-Qaeda affiliate based in Somalia, has been behind a series of high-profile attacks including the Westgate shopping centre siege in Nairobi in 2013, and a violent assault on a university earlier this year in which nearly 150 people were killed.

HABARI ZA HIVI PUNDE!

Maelfu ya watu wamehudhuria misa ya waamerika 9weusi waliopingwa risasi,katika jimbo la South Carolina.

Friday, June 19, 2015

'RAIS OBAMA AKERWA NAMAUWAJI MAREKANI'

Rais Barak Obama amesema mauaji ya watu tisa ndani ya Kanisa la Waafrika Wamarekani katika eneo la Charleston katika jimbo la Carolina Kusini yanaibua maswali kuhusu sehemu mbaya ya historia ya Marekani.
Katika hotuba yake iliyoonyeshwa katika televisheni muda mfupi baada ya polisi kumkamata mtuhumiwa ambaye ni kijana wa kizungu-- Bwana Obama amesema chuki miongoni mwa jamii kwa misingi ya rangi na imani ni kitisho kwa demokrasia ya Marekani na misingi yake.
Amesema mauaji ya watu wengi hayatokei kwa kiasi hiki katika nchi nyingine zilizoendelea, na ametaka kufanyika kwa mabadiliko ya pamoja katika fikra za Wamarekani kuhusu ghasia zinazosababishwa na matumizi ya silaha.